Hapo zamani, imani na utamaduni vilirisishwa sana kwa njia ya kuzungumza, yaani oral tradition. Na hivyo maagano hayo ya wakati huo yametafsrika katika Kanisa la leo kama Agano la Kale. Lakini Stephano anazungumza juu ya Agano la mioyo; hili ni Agano ambalo Mungu anazumza na wanadamu na analiweka Yeye mwenyewe. Hakuna mtu ambaye anahusika hapo katikati kuliweka hilo Agano isipokuwa ni Mungu mwenyewe kwa njia ya Yesu Kristo. Na amelithibitisha Agano hilo kupitia unabii wa Yeremia katika sura 32: 40.
Nilipotazama neno kicho katika Neno hilo, kwa tafsri ya Kiebrania, lilitafriwa kama an object that cause fear, yaani kitu kinachoweza kusababisha hofu. Mungu anajitokeza kwa njia ya Yesu Kristo kuanzisha Agano la mioyo ndani ya mwanadamu; na humo ndani ya mwanadamu anawekeza kitu kinachoitwa kicho, kitu kitakachomletea mwanadamu hofu, ili kila wakati anapofikiri kumuacha Mungu kile kitu kinamkumbusha. Lakini hicho kitu hakikuwa kitu tu baada ya Kristo, ni Roho Mtakatifu; Yeye anatukumbusha ili kila wakati tutakapofikiri kumuacha Mungu anaturejesha kwake. Ndugu zangu, lakini ipo gharama ya kuwa shahidi halisi…”