Imani ya Mitume au Imani ya NIKEA ni kauli (Tamko) ya imani, au kiapo cha imani, SIYO sala; ni tamko la ukweli, sawa na kiapo cha uaminifu kwa Kristo na utume wake. Tamko hili linarejea imani ya msingi ambayo mitume walishikilia, walihubiri, na kufa kwa ajili yake.
Ni tangazo linalotoa muhtasari wa imani kuu za Ukristo. Ni kiapo cha utii kwa Kristo, ambacho mitume walibaki nacho, tena wakiwa thabiti katika imani yao licha ya mateso na kifo (vifo) cha imani.
Leo hii, makanisa mbalimbali ulimwenguni hukiri imani hii katika matukio mbalimbali:
- Viapo vya Ubatizo – Kutangaza imani kabla ya ubatizo.
- Viapo vya Kidini – Mapadre, Wachungaji, na wamisionari hula kiapo cha uaminifu kwa Kristo na Kanisa Lake.
- Maungamo ya Imani – Katika nyakati za mateso, Wakristo wamekufa huku wakitangaza, “Yesu ni Bwana!” (Warumi 10:9).
Tumsikilize Baba Mchungaji akielekeza namna ya ukiri wa Imani hii. Bofya kiunganishi hiki