“Ni Damu Idondokayo” ni wimbo ulioandikwa na William Cowper (1731–1800), mzaliwa wa Berkhamsted, Uingereza. Chimbuko lake ni Kitabu cha Zekaria 13:1, inayoeleza juu ya kisima kilichofunguliwa kwa ajili ya kutakasa dhambi. Cowper aliandika wimbo huu akiwa kwenye kipindi kigumu cha msongo wa mawazo. Alipambana na ugonjwa wa akili kwa muda mrefu wa maisha yake; wimbo huu unaonesha imani yake kubwa katika damu ya Yesu Kristo inayookoa. Maneno ya wimbo yanaeleza tumaini, wokovu, na nguvu ya utakaso kupitia dhabihu ya Yesu.
Historia inaonesha kwamba William alimpokea Kristo baada ya kupatwa na mfadhaiko mkubwa wa akili na akapata faraja katika imani. Licha ya changamoto hii, tunamkumbuka kama mmoja wa waandishi bora wa nyimbo za Kikristo katika historia. William Cowper alikuwa ni rafiki mkubwa wa John Newton, mwandishi na mtunzi wa wimbo unaofahamika sana – BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA. Wawili hawa walishirikiana kuandika kitabu cha nyimbo Olney Hymns (1779), ambacho kilijumuisha wimbo huu; NI DAMU IDONDOKAYO.
Katika majira haya ya Kwaresma, tukumbuke pendo kubwa la Bwana wetu Yesu Kristo tukiimba Ni Damu Idondokayo Mwilini mwa Yesu. Bofya kiunganishi hiki:
