Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Latest Posts

UNAIFAHAMU ASILI YA KANTATE DOMINO?

“Cantate Domino” (au “Kantate Domino”) ni maneno yanayomaanisha “Mwimbieni Bwana”, ni agizo la kibiblia kama tusomavyo katika Zaburi 96:1 na 98:1 – ambazo zote  huanza na maneno Mwimbieni Bwana wimbo mpya yaani,“Cantate Domino canticum novum.”na pia Zaburi 149:1 inayoanza na Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya.

Chimbuko la jina la Jumapili ya Cantate (Jumapili ya nne baada ya Pasaka katika kalenda ya liturujia) ni kutokana na maneno ya mwanzo ya wimbo wa introit, yaani, “Cantate Domino.” Maadhimisho ya siku hii tunayaona katika nyimbo za Kanisa Katoliki, Kilutheri na Anglikana, pamoja na vitabu vya sauti za kwaya na sala.

Zaburi za 96; 98 na 149 hutumika sana katika ibada na zimekuwa msukumo wa nyimbo mbalimbali za kwaya na muziki wa kitamaduni wa Kikristo. Baadhi ya watunzi wa muziki wa kawaida (classical) wameandika nyimbo zenye jina Cantate Domino, kama vile; Giuseppe Pitoni, Heinrich Schütz, Claudio Monteverdi na Arvo Pärt – Alichapisha toleo maarufu mwaka 1996 lililo na mchanganyiko wa Kilatini na mitindo ya “Gregorian”

Zaburi ya 148 iliyosomwa leo katika mahubiri kwa mujibu wa Kalenda ya Kanisa ina historia kubwa sana. Baadhi ya wanazuoni (hasa katika maandishi ya apokrifa kama vile Sala ya Azaria na Wimbo wa Watoto Watatu Watakatifu unaopatikana katika Septuagint ya Kigiriki) wanaamini kwamba Daniel aliimba wimbo wenye maneno sawa na Zaburi hii pale alipotupwa katika tundu la simba na hata kutaka kuangamizwa kwa moto.

Sehemu ya wimbo wake inasomeka hivi: “Mhimidini Bwana, enyi kazi zote za Bwana, mwimbieni sifa, mtukuzeni milele. Mhimidini Bwana, ewe moto na joto.” – ubeti huu ukapelekea moto usiwadhuru! Wimbo ukaendelea kuamuru hata Wanyama wakali wamsifu na kumuimbia Bwana. Nao wakatulia. Daniel na wenzake wakatoka huru

Mataifa yote yanamsifu Mungu. Viumbe vyote vinamsifu Mungu. Mungu wetu amekaa katika sifa – tunapoazimisha Kantate hii, karibuni tumsifu kwa kumuimbia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*