Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Latest Posts

TUZIJUE NYIMBO ZETU – YESU MWOKOZI

Wimbo YESU MWOKOZI ulionekana kwa mara ya kwanza katika chapisho la nyimbo za Kikatoliki – 1677 Munster Gesangubuch, ambapo majina halisi ya mtunzi hayakuandikwa. Hata hivyo, masimulizi yanaonesha kwamba katika vilima vya Silesia, katika kijiji kidogo kilichozungukwa na malisho mazuri ya mifugo, mchungaji mmoja, kijana mdogo, wa wanyama alikuwa akichunga kundi lake.

Jioni moja, baada ya siku ndefu, aliketi chini ya mti wa mwaloni, akitazama machweo ya jua yakionyesha kijito kilicho karibu. Mawazo yake yakajielekeza kwenye uzuri wa uumbaji — milima, maua na anga. Moyoni mwake alijua kwamba hakuna kitu kinachoweza kulinganishwa uzuri wake na uzuri wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Ndipo akaanza kuimba wimbo huu; “Schönster Herr Jesus, Herrscher aller Herren, Gottes na Marien Sohn…” Yaani “Bwana Yesu mzuri sana, Mtawala wa Mabwana wote, Mwana wa Mungu wa Mariamu…”

Alipokuwa akiimba, wanakijiji waliokuwa wakipita walivutiwa na sauti yake. Baada ya muda, wimbo huo ulienea zaidi ya kijiji, ukibebwa na mahujaji na wasafiri. Wimbo huu uliingia katika makanisa na nyimbo za dini, ukawa wimbo unaopendwa sana ulioimbwa kote Ulaya.

Baadaye wimbo huu ukawa wimbo wa sifa usio na wakati, ukiwakumbusha vizazi kwamba uzuri wa Kristo unapita vitu vyote duniani. “Schönster Herr Jesus” ukapendwa na kutumiwa sana na Wajesuiti katika karne ya 17 – Wajesuit au Jumuiya ya Yesu (Societas Iesu, S.J.), ni shirika la kidini la Kikatoliki la lililoanzishwa mwaka wa 1540 na Mtakatifu Ignatius wa Loyola, pamoja na masahaba sita, akiwemo Mtakatifu Francis Xavier. Wajesuti wanajulikana kwa kujitoa kwao katika elimu, kazi ya umishonari, teolojia, sayansi na falsafa. Wengine hulitambua shirika hili kama Shirika la Kijasusi la Kikatoliki – “Catholic Intelligence Service.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*