Kama mkristo, maombi lazima yawe sehemu ya maisha yako. Tenga muda wa maombi, tena ya faragha; nje ya maeneo ambayo umeyazoea. Tafakari mwenyewe, omba mwenyewe. Ushindi wako uko katika maombi. Katika maombi unakiri kwamba wewe huwezi; unamwambia Mungu bila Wewe, mimi siwezi, naye atatenda. Nyenyekea kwake.