Mchakato wa kufikia mwisho mwema unaweza kuwa mchungu. Limao si tamu mdomoni; ukipewa limao, tengeneza juisi yake. Kwa hiyo usifikirie uchungu wa hilo limao bali fikiria utamu wa juisi yake. Hii itakupa nguvu ya kusonga mbele. Na nguvu yako kama mkristo unaipata kwa Yesu Kristo aishiye milele. Magumu unayopata yatakupa matokeo mazuri kwa sababu nyakati na majira yako katika Mungu mwenyewe. Every cloud has a silver lining. Usihudhunike katika njia yenye magumu unayopitia, yafurahie mapigano, kwa sababu Mungu anapigana pamoja na wewe. Hakika lazima utafikia lengo kwa kuwa umemtanguliza yeye kupitia maombi