Kwaya ya Vijana ya Usharika imeshiriki katika uimbaji wa nyimbo sanifu ngazi ya Jimbo, ambapo Jimbo la Kaskazi la Dayosisi ya Mashariki na Pwani KKKT uimbaji uliganywa katika vituo viwili: Kituo cha Madale Bethel na Boko. Kwaya ya Vijana Msasani ilipangwa katika kituo cha Madale Bethel na kuibuka mshindi wa Pili katika kituo hicho.
Wimbo wa mashindano ulikuwa ni NJOO MSALABANI katika Kitabu cha TMW Wimbo Namba 93.